Mwanamume aliyeteka nyara ndege ya shirika la Misri la EgyptAir na kuishurutisha kutua Cyprus amekamatwa, wizara ya mashauri ya kigeni ya Cyprus imetoa taarifa.
Katika harakati za kuiteka ndege hiyo mwanamume alitishia kua amejifunga mkanda wa kujilipua hivyo alimtaka rubani wa ndege kuielekeza ndege hiyo Cyprus au Uturuki
Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Alexandria kuelekea Cairo ambapo ilikuwa na abiria 21 wa kigeni wakiwemo Wamarekani wanane, Waholanzi wanne, Waingereza wanne na Mfaransa mmoja.
hata hivyo Rubani alilazimika kuitua ndege hiyo katika uwanja wa Larnaca nchini Cyprus, ambapo takribani abira wote walifanikiwa kuondoka kutoka kwenye ndege hiyo.
Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir alikua akihitaji kuongea na mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amesema kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege ilioandikwa Kiarabu akiomba ipelekwe kwa mtalaka wake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni