Habari na Ephraim Mkali Banda,
Rais wa Malawi - Peter Muthalika |
Polisi nchini Malawi wana mshikilia mwanafunzi moja
wa chuo cha Tekinolojia mjini Lilongwe Patric Semu kwa kosa la kumtukana rais
Mutharika wa inchi hiyo,
Tarifa kutoka katika jeshi la polisi nchi Malawi iliyo
tolewa na Msemaji wa jeshi hilo Bw. Nicholas Gondwe amesema mwanafunzi huyo
alikamatwa katika barabara ya kenengo ambapo polisi wa Usalama barabarani walisimamisha
dalala dalala aliyokua amepanda kijana huyo kupisha musafara wa rais Mutharika
uliye kua ukielekea kwenye ufinguzi wa ujenzi wa chuo cha madaktari mjini
Lilongwe,
Gondwe alisema kijana huo alitoa lugha ya matusi baada
ya polisi kusimamisha magari kupisha msafara wa mkuu wa nchi hiyo.
Patrick mwenye umri wa miaka 19 atajibu mashitaka
yakutoa matusi kwa rais kwa kulingana na sheria ya 182 ya kuendesha shitaka
hilo. Adhabu ya kosa hilo ni kwenda jera miezi sita,
Mwaka jana mzee moja wa miaka 62 katika wilaya ya
Balaka alilipa kiasi cha Kwacha elfu tatu hela ya kimalawi kwa kosa kama hilo.
Kijana huyo alisema rais Mutharika ameshindwa
kuongoza nchi hiyo na ameshindwa kabisa kutatua tatizo la njaa linalo ikumba
nchi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni