JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS.
Mtakumbuka
kwamba leo ni siku ya 15 ya utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa la kuwataka kuwaondoa
kwenye malipo watumishi hewa.
Natumia
fursa hii kutoa taarifa kwa Umma kuwa Agizo hilo limetekelezwa kama Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza.
Taarifa
za watumishi hewa tayari zimewasilishwa kwa maandishi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
kuanzia mwishoni mwa wiki.
Kwa
sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi na zitakapokuwa tayari kwa matumizi ya Umma
zitatolewa kwa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuufahamisha Umma.
Hivi
sasa taarifa hizi zinakusanywa kwa pamoja ili kupata idadi kamili.
Wakati
huo huo, napenda kuufahamisha Umma kuwa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam
(DART) yameanza kufanya mazoezi ya utoaji huduma toka siku ya alhamisi tarehe
24/03/2016. Tunategemea wiki hii mtoa huduma ataendelea kuongeza idadi ya
mabasi ya kufanya mazoezi kabla zoezi hili halijaanza rasmi.
Imetolewa:
George
B. Simbachawene (Mb)
Waziri
wa Nchi
29/03/2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni