Machifu wakiwa katika mkutano katika Hotel ya Grand Paris mjini Mzuzu - Malawi |
Ma chifu wanao tokea
kusini mwa nchi ya Malawi wameibeba serikali ya Mtharika kwa kusema matatizo ya
kiuchumi yanayo ikumba nchi hiyo yanatokana na ubadhirifu wa fedha uliotokea
katika utawala wa Bingu Wamtharika na Joyce Banda.
Hayo yamezungumzwa na Ma
chifu katika mkutano wao wa kujadili mambo mbali mbali ikiwemo matatizo yanayo
ikumba nchi ya Malawi,
Wakizungumza na wandishi
wa habari, chifu Mpherembe, Fukamapiri, Mkumbira, Mwahenga na Mwankhunikira
walisema tatizo la njaa linalo ikumba nchi hiyo hivi sasa halijasababishwa na serikali
bali ni mabadiliko ya tabia ya nchi ndio sababu kuu,
“Ni makosa sana wana siasa
kusimama ma jukwani na kuanza kumlaumu rais Mutharika kua anahusika na janga la
njaa, kwani hamjasoma jiografia kwamba kuna mabadiliko ya tabia ya nchi? tumekerwa
sana na kelele zenu majukwani, kinachotakiwa kwa sasa ni kusaidia serikali
kutatua matatizo kwa pamoja sisi kama viongozi wa mila hatukubaliani na mawazo
ya vyama vya upinzani Malawi Congress Party MCP, People's Party PP na Allaence
For Democracy AFORD na asasi nyingine kwamba rais Mutharika asipotatua matatizo
ya uchumi na njaa ndani ya siku 90 atapaswa kuachia madaraka, rais anachaguliwa
na wananchi sio asasi wala chama chochote kile ni wananchi wanaomuweka rais
madarakani,” alisema mmoja wa machifu hao.
Machifu ni watu wanawo
heshimiwa sana katika inchi ya Malawi na ni watu wenye sauti kubwa kwa jamii,
asasi zingine za serikali na vyama vya siasa,
Aidha kufuatia kauli hiyo
ya machifu vyama vya upinzani vimesema huenda Machifu hao wametumwa na serikali
ya Mtharika kusema hivo. Ikumbukwe kua Mwenyekiti wa vijana wa ki Malawi
waishiwo nchini Tanzania bwana Griffin Botha alinukuliwa akisema ni wananchi
nchi pekee katika nchi ya Malawi wenye uwezo wa kumuondoa rais madarakani sio
chama wala asasi.
Kwa hatuwa hii ya Machifu
kutoa tamuko lao ni imepelekea vyama vya upinzani nchini Malawi kukosa nguvu
katika adhimio lao na ushawishi kwa wananchi kwa kua wananchi nchini humo
huwaamini machifu, Pia Machifu hao
katika mukutano wao huo katika hoteli ya Grand Paris mjini Mzuzu waliwataka
wana nchi kupuuza matamuko ya watu wanao taka kuvuruga amani ya inchi hiyo.
Rais wa Malawi Prof. Piter Mutharika |
Wakati huo huo Chifu Zwangendaba
Jere Ngoni kutoka Wilaya ya Mzimba nchini Malawi imeomba idara ya serikali
nchini Malawi inayohusika na utamaduni kujifunza kutoka katika serikali ya
Tanzania kudumisha na kueneza utamaduni kwa kutoa sapoti kwenye sherehe za
utamaduni.
Akizungumza kwa niaba ya
machifu, Katibu wa tasisi ya Mzimba Heritage Association bwana Ndabazeke baada
ya kuwasili nchi Malawi akitokea nchini Tanzania katika sherehe na kumbukumbu
za Mapinduzi ya Maji Maji yaliyofanyika Songea, Tanzania
Maadhimisho hayo
yalifanyika mwishoni mwa juma lililo pita. Thole ambaye pia alikua mmoja miongoni
mwa wa Ngoni kutoka Malawi walio hudhulia maadhimisho hayo akiwa na Chifu
M'mberwa namba tano, Chifu Mtwalo, Kampingo Sibande na Jalavikuba alisema
serekali ya Tanzania ili chukua jukumu kubwa katika maadhimisho hayo ya Maji
Maji.
“Serikali ya Tanzania ili husika sana kwa
kuandaa maadhimisho hayo licha ya kua kwamba Maji Maji ilikua ni vita kati ya
wa Ngoni na Ujerumani, Tungependa serikali ya Malawi iige mfano nzuri kwa
serikali ya Tanzania kwa kutoa msaada katika ku enzi utamaduni, alisema Thole,”
Maji Maji ni mahadhimisho yanayo fanyika kwa
kuwakumbuka na kuwa enzi wa Ngoni walio kufa nchini Tanzania katika mapigano yakutaka
kujitawala dhidi ya Wajerumani.
Thole pia alisema Mzimba
Ngoni ina vitu vingi ambavo vinaweza kuvuta watali, lakini serikali haijaliona
hilo kwani hadi sasa hatuwezi kusema serikali imesaidia licha ya viongozi
wenyewe kufanya jitihada zeo za kutunza naku enzi utamaduni wetu.
Katibu wa Mzimba Heritage Association NGONI, Bw. Ndabazeke Thole |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni