Polisi nchini Malawi wanasema kundi moja la watu limewauwa watu saba kwa
kuwachoma moto kwa madai ya kukutwa na viungo vya binaadamu wenye ulemavu wa
ngozi (albino) kwa ajili ya matumizi ya kishirikina.
Mkuu wa polisi wa wilaya ya Nsanje iliyopo kusini mwa nchi ya
malawi, Kirdy Kaunga, amesema kundi la watu hao waliamua
kujichukulia sheria mkononi kwa kuwawasha moto wakitumia mafuta ya petroli
baada ya kuwa kuta watu hao saba na mifupa inayodhaniwa kua ni mifupa ya watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Afisa huyo wa jeshi la polisi nchini humo amesema bado
wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini kama mifupa hiyo ilikuwa ni
ya watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino.
Katika nchi kadhaa za Kiafrika, zikiwamo Malawi, Msumbiji na
Tanzania, watu wenye ulemavu wa ngozi huandamwa kwa mashambulizi yanayolenga
kukatwa viungo vyao ambavyo hutumiwa kwenye mambo ya kishirikina.
tunaomba radhi kwa picha hizi, lengo ni kua na uhalisia wa tukio,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni