NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na
Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amekutana na Afisa
miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa
Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile katika mazungumzo yaliyofanyika leo asubuhi
Aprili 14.2016, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Kigwangalla ameomba Tanzania
ipatiwe kibali cha kununua mashine mpya ya kutibu saratani (LINAC) Sambamba na
sehemu ya msaada iliyoahidiwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw.Yukiko Amano mbele
ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Mizengo Kayanda Pinda miaka mitatu iliyopita.
Tanzania tayari imetenga kiasi cha Euro 1.65 Milioni kwa
ajili ya kukidhi mahitaji ya mchango wake kwa asilimia 50 kama mradi ulivyokuwa awali, Mh. Kigwangalla alisema: “Bahati mbaya sana kutokana na
ucheleweshwaji, Bajeti ya msaada huo kutoka IAEA ilipitwa na wakati na kusababisha Tanzania kukosa fursa hiyo.
Malengo ya Tanzania ni kununua mashine hizo mbili kwa ajili ya kuboresha huduma za tiba ya
Mionzi nchini”.
Ujenzi wa jengo kwa ajili ya kufunga mashine hizo mbili
umesha kamilika na mashine moja itakamilika mwaka huu na ya pili mwakani ili
kuboresha huduma za Saratani nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni