WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
TAMKO LA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
KULAANI KUBAKWA NA KULAWITIWA KWA MTOTO KATIKA MANISPAA YA MIKINDANI, MKOANI
MTWARA.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa
na kukemea vikali tukio la mzazi kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kufikia
mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, kitendo kilichofanywa na John Donald (35)
mkazi wa Kiyangu, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara.
Tukio hili la kubaka na kulawitiwa ni ukatili wa hali ya juu dhidi ya
mtoto maana husababisha maumivu makali ikiwa ni pamoja na kumdhuru mtoto
kimwili, kisaikolojia, kijamii na kihisia. Aidha, vitendo hivi, vinaacha kovu
la kudumu kimwilini, kiakili, kimaadili, kijamii, ulemavu, maumivu, na wakati
mwingine husababisha kifo; jambo ambalo linahitaji ulinzi thabiti katika
kuhakikisha watoto wanaishi mazingira salama na rafiki.
Ukatili alilofanyiwa mtoto eneo la Kinyangu, manispaa ya Mikindani, ni
ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto ambao huchangia kurudisha nyuma ustawi na
maendeleo ya Mtoto na ni kinyume cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.
Wizara inatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara kwa kumkamata
mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe. Vile
vile, Wizara inaipongeza Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es salaam
dhidi ya Omary hamisi (25), mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es salaam, ya
kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti
mtoto wa miaka tisa mwenye ulemavu wa kusikia na kuongea.
Uamuzi huu ni kielelezo kuwa, wananchi wakitoa ushahidi wa matukio ya
ukatili dhidi ya watoto, watuhumiwa watachukuliwa hatua kali ili kuwa fundisho
kwa wananchi wanaowanyanysa watoto. Wizara inamwelekeza Afisa Ustawi wa Jamii
na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Mtwara kuwasiliana na wadau wengine
katika ngazi zote kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma ya afya na ushauri
na kufuatilia mwenendo wa shauri hili.
Imetolewa na
Erasto Ching’oro
Msemaji
wa Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni