Mwalimu Mkuu Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya amefikisha Mahakamani kwa tuhuma za kumpachika mimba mwanafunzi wake wa darasa la saba
Na Frederick siwale mbarali mbeya
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Utyego iliyopo
katika Kata ya Ubaruku Wilaya ya Mbarali mkoani mbeya, amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wake.
Mtuhumiwa Shusha M Wameambiwa (45) ambaye ni Mwalimu
mkuu wa shule hiyo, amepandishwa kizimbani mbele ya hakimu mafawidhi wa
mahakama ya Wilaya ya mbarali Agenesi Ringo kwa tuhuma za kupatia mimba
mwanafunzi wake wa darasa la saba a (jina lake linahifadhiwa) nayesoma katika shule hiyo ya Utyego.
Akizungumza na muandishi mahakamani hapo afisa Ustawi wa Jamii Wilaya
Winfrida mahali, amesema kitendo alichofanya mtuhumiwa ni ukatiri wa kijinsia.
Naye afisa ustawi wa Jamii anayeshughulikia
kitengo cha mahakama David Makele, amesema vipimo vya madaktari vinaonyesha
kuwa ujauzito huo una umri wa miezi nane na nusu.
Aidha mkurugenzi wa shirika la kupinga ukatili
dhidi ya watoto na Wanawake Tanzania (SHIKUMWATA) Leopard Kitalima, amesema
Wilaya hiyo inakabiliwa na wimbi kubwa la Vitendo vya ukatili na unyanyasaji
kwa watoto na Wanawake na kudai kuwa changa moto kubwa ni kukosekana kwa elimu
ya sheria na haki kwa jamii.
Mashitakiwa mwampamba yupo nje kwa dhamana hadi
mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoletwa tena
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni