Ijumaa, 13 Mei 2016

Ndani ya siku 7 Gadner anatakiwa awe amemuomba radhi mtalaka wake Lady Jay Dee,









Juma lililopita Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Khamisi Andrea Kigwangalla aliingilia kati Ugomvi wa Judith Daines Wambura Mbibo(Lady Jay Dee) na aliyekuwa Mume wake Gadner .G. Habash.

Kupitia mtandao wa kijamii Naibu Waziri alitoa rai kwa uongozi wa Clouds Media kumsihi Gadner amuombe radhi msanii Lady Jay Dee, kufuatia kauli aliyoitoa mbele ya kadamnasi akimtusi mke wake wa zamani Lady Jay Dee.

"Ndg. Gardner amefanya udhalilishaji mkubwa si tu kwa Jide Jaydee bali ametukana Wanawake wote. Mimi Balozi wa wanawake namtaka aombe radhi"

Natoa rai kwa uongozi wa Cloudsfm kumtaka Ndg. Gardner afute kauli yake na aombe radhi kwa Jide Jaydee na kwa umma ili kulinda heshima yao" Kigwangallah amesema.



Hata hivo kauli ya Gadner ilizua gumzo karibu katika mitandao mingi ya kijamii hususani WhatSapp kufuatia kipande cha sauti ambajo Gadner alisikika akisema kua hana neno ya yule mtoto wa kike kwa kua amesha mkojoza kwa miaka 15 ,  

Wikiendi iliyoisha kuna video ilisambaa mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.

kauli hiyo ilitafsiriwa kua niya udhalilishaji dhidi ya Lady Jay Dee na wanawake wote kwa ujumla ambapo baadhi ya  mashabiki wa Lad Jay Dee wakiwemo wanaumekwa wanawake walione kukerwa na kauli hiyo!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni