Alhamisi, 12 Mei 2016

Wafanyabiashara tisa (9) Mkoani Arusha wakamatwa kwa kosa la kuuza sukari kinyumbe na bei elekezi ambayo ni sh.1800/=


Polisi mkoani Arusha inawashikiliwa wafanya biashara tisa (9) kwa baada ya kubainika wakiuza sukari kinyume na bei elekezi ya serikali ambayo ni sh. 18,00

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema leo kua watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi.
Mkumbo amesema wafanya biashara hao walikutwa wakiuza sukari kwa ghalama kati ya  Tsh 6,200 5,000, 4500, 3000 na 2500, kwa kilo moja.

Aidha kamanda amewasihi wafanya biashara kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na serikali na kuwatahadharisha kua serikali itaendelea kuwakamata watu wote wanaouza sukari tofauti na bei elekezi na kwamba kamatakamata hiyo ni endelevu.

Ikumbukwe kua msako huo au kamatakamata dhidi ya wafanyabiashara wanaoficha sukari unaendeshwa na maofisa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Polisi,

Aidha msako huo ulianza baada Rais John Pombe Magufuli kutoa agizo hilo wiki iliyopita.

Kufuatia changamoto ya upatikanaji sukari nchini serikali ililazimika kuagiza tani 70,000 kutoka nje ambapo hadi sasa imeanza kupokea sukari kutoka nje ikiwa ni sehemu ya tani 70,000/ ili kukabiliana na uhaba uliopo huku ikiwataka wasambazaji kuiuza kwa sh 1,800.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana alisema kua tayari tani zaidi ya 11,000 zimewasili nchini ambapo leo zimeanza kusambazwa katika mikoa yote huku tani zaidi ya 20,000 zikitarajiwa kuwasili ijumaa hii. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni