Na.Mwandishi
wetu,Bahi
Waziri Ummy Mwalimu akiwasili kwenye kituo cha afya Mundemu wilayani Bahi. |
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amewahimiza
wananchi wa wilaya ya Bahi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili
kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.
Waziri
Ummy alisema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani BAHI ambapo
kwa kutembelea kituo cha Afya cha Mundemu.
Akijibu
maswali ya wananchi kuhusu kutopewa dawa licha ya wao kuwa na kadi za CHF,
Waziri Ummy amewahakikishia wananchi wote kuwa, wizara yake kupitia Bohari ya
Dawa(MSD) itahakikisha dawa za kutosha zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma
ili wananchi na wanachama wa CHF waweze kupata dawa wakati wote."kupitia
CHF iliyoboreshwa mtaweza kupata huduma hizo hadi ngazi ya Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa"alisema
Katika
ziara hilo,Waziri Ummy pia alitembelea mradi wa usafi wa mazingira mashuleni,
katika jamii na maeneo ya kutolea huduma kwa jamii unaofadhiliwa na PLAN
INTERNATIONAL.
Mmoja wa watumishi wa kituo hicho akimsomea taarifa ya kituo hicho cha afya waziri wa afya(hayupo pichani). |
Waziri wa afya akiongea na wagonjwa walifika kituoni hapo kupata huduma(picha na Habari na wizara ya afya. |
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kituo hicho cha afya |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni