Jeshi la Polis kanda Maalumu jijini Dar es salaam limekamata
watuhumiwa sugu 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia
nguvu, wizi wa maungoni, wapiga debe, wavuta bangi, kikosi cha mbwa mwitu,
watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali
jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na kamishina wa polisi kanda maalumu ya Dar es
salaam Simon Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo,
Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya
operesheni kali katika maeneo mbalimbali jijini humo.
Aidha pamoja na kufanikisha zoezi hilo kwa watuhumiwa hao,jeshi
hilo pia wamekamata lita 952 za pombe aina ya gongo,bangi puli 227, kete 210,
na misokoto144 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Katika hatua nyingine ,kikosi cha kupambana na wizi wa simu
cha polisi kimefanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa watatu(3) kwa makosa ya
uporaji wa simu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kinondoni,watuhumiwa hao ni
Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36),Abdallah Said (22) wote wakazi wa
jijini Dar es salaam.
Hata hivyo kamanda Sirro aligusia zoezi zima la uhakiki wa
silaha na kusema kuwa lilienda vizuri na watu walijitokeza kwa wingi japo kuna
changamoto kadhaa zilizojitokeza ’’zoezi lilifanyika vizuri ingawa kulijitokeza
dosari ndogo ndogo’’alisema kamanda Sirro.
Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya
Dar es salaam limeweza kujikusanyia kiasi cha shilingi 562,860,000/=
kutokana na ukamataji wa makosa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia tar
15/7/2016 hadi 21/7/2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni