Ijumaa, 22 Julai 2016

Waziri Ummy Mwalimu, azindua ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya Gairo!!

Na.Catherine Sungura,Gairo
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi ya wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya Gairo.

Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wametakiwa kuweka kwenye mipango yake na kiwe kipaumbele chao  ujenzi wa Hospitali ya wilaya.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi  inayojengwa kwenye kituo cha Afya mjini hapa inayodhaminiwa na mbunge Ahmed Shabiby.

Waziri Ummy amesema wodi hiyo ikikamilika itawasaidia akina mama wengi wa halmashauri Hiyo pamoja na vijiji vya jirani  kufika kituoni hapo kujifungua"suala ya uzazi kwa mwanamke ni haki yake ya msingi,hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao pia na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua" 

Aidha,amesisitiza juu ya utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa akina mama wajawazito,wazee na watoto chini ya miaka mitano.
"Nazikumbusha hospitali na vituo vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi haya,pia muweke  dirisha litakaowahudumia wazee,na hii ndio muhimu mlitekeleze" 

Kwa upande wa watumishi,Waziri Ummy Karnataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria na taratibu Za taaluma zap na kuzingatia viapo vyao katika kuwahudumia wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo.miongoni mwao.
"Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri  uhakikishe unatatua changamoto za watumishi ikiwemo kuwalipa posho za sare za kazi,  likizo na stahiki zao nyingine watumishi hawa"

Awali akisoma taarifa ya Wilaya,mkuu wa wilaya hiyo bi. Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya Wilaya Mkuu wa wilaya ya Gairo juu ya hali ya huduma za afya wilayani humo, alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwemo ukosefu wa hospitali ya wilaya,  gari la kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefu.

Waziri Ummy Mwalimu akiwasikiliza watumishi wa kituo hicho cha afya(hawapo pichani),kushoto ni mbunge wa jimbo la Gairo Mhe.Ahmed Shabiby(wa kwanza kushoto)Mkuu wa Wilaya hiyo mhe.Siriel Mchembe(wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri  bi.Agnes Mkandya.

Waziri wa afya akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo,mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha afya gairo(picha na wizara ya afya)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni