Hapo jana blog hii iliandika taarifa za kukamatwa kwa bw. Zacharia Benjamini mwenye umri wa miaka 35 kwa tuhuma za kuingia katika hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro na kujifanya daktari ili hali hana taaluma hiyo.
Taarifa za awali toka kwa jeshi la polisi mkoani Morogoro zinasema
mtuhumiwa Benjamini alikua na lengo la kutaka kufanya uhalifu wa kutapeli na kwamba mtuhumiwa aligunduliwa na mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi hospitalini hapo.Taarifa za awali toka kwa jeshi la polisi mkoani Morogoro zinasema
Mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa alidai yeye ni mwanajeshi, askari mstaafu, polisi na pia aliwahi kuwa mganga hivyo hazuiliwi kuingia popote anapotaka.
Akielezea tukio hilo jana kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jumapili iliyopita majira ya saa 11 katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika hospital hiyo.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutembelea wodi zote tisa na baadae kuingia wodi ya wagonjwa mahututi, awali mtuhumiwa huyo alipofika aliingia wodi namba saba chumba cha manesi na kuchukua koti la mganga kisha kulivaa ili asiweze kugundulika.
Akiwa wodini mtuhumiwa alijitambulisha kuwa yeye ni daktari mgeni anayekagua wagonjwa kama wanapata huduma ipasavyo ambapo baada ya kuingia chumba cha wagonjwa mahututi alianza kuwahoji wagonjwa na ndipo mmoja wa wagonjwa aliekua na nafuu alipopiga simu polisi na kutoa taarifa juu ya mtu huyo ambaye alikua akimshuku kuwa sio daktari ndipo polisi walimkamata na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Akizungumzia tukio hilo muuguzi wa zamu Esther Uwiza amesema mtu huyo aliingia wodi namba moja akiwa hana koti la udaktari na baadaye akaenda wodi namba saba na chumba cha kubadilishia nguo ambako alichukua koti la udaktari na kulivaa na kwenda chumba namba tisa kabla ya kukamatwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dr. Frank Javob amethibitisha kutokea kwa tukio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni