Na.Mwandishi
wetu,Addis Ababa
Mhe Ummy Mwalimu akiwa na waziri wa afya (Uganda) Mhe .Sara Opendi na Mhe Omar Sey Waziri wa Afya wa Gambia. |
Ugonjwa wa saratani nchini Tanzania ni chanzo cha magonjwa na
vifo,hivyo inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika
kila mwaka.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika
Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti
na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini hapa.
Waziri Ummy amesema
kati ya wagonjwa hao asilimia 38 ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa
wanawake, asilimia 14 saratani ya ngozi, asilimia 10 saratani ya matiti na saratani
ya tezi ni asilimia 4 Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka
kutokana na magonjwa ya Saratani.
Licha ya changamoto
mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo
uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa tiba, Uhaba wa Watumishi
wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za dawa za matibabu ya
saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya Tanzania imepitisha Sera za Kitaifa na
Miongozo mbalimbali ya Kupambana na Saratani, kutoa Elimu kwa jamii na watoa huduma
za afya nchini kuhusu Saratani.
Aidha, kuanzishwa kwa
huduma za upimaji wa saratani katika Hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300
nchini na huduma za Tiba kupitia Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
"Serikali
itapanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando Mwanza na
KCMC, Kilimanjaro. Mipango ya baadae ni huduma hizo pia kutolewa ktk Hospitali
ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya."hii itapunguza wagonjwa kufuata huduma kwenye
hospitali ya saratani ya Ocean Road Mkutano wa 10 wa Saratani ya shingo ya
kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unafanyika kwa kuasisiwa kwa juhudi
za wake za Marais wa bara la Afrika.
Mkutano huu
unahudhuriwa na Wake wa Marais wa Afrika, Mawaziri wa Afya wa Afrika,
Wanataaluma na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu ni kufanya mapitio ya hatua
zilizochukuliwa na nchi za Afrika, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya
pamoja na ya nchi katika kukabiliana na saratani. Wakati wa kukabidhiwa
uenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na saratani ya
Shingo ya Kizazi, Matiti na Tezi Dume kutoka kwa Mwenyekiti anaemaliza muda
wake, mke wa Rais wa Kenya mama Magreth Kenyatta, Mke wa Waziri Mkuu wa
Ethiopia mama Roman Tesfaye Abneh ameleeza masikitiko yake kwa jinsi ambavyo
ugonjwa wa saratani unavyoua kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu.
Hivyo ameziomba nchi
za Afrika kuongeza uwekezaji katika eneo hili hasa kwa kuhakikisha dawa
zinakuwepo za kutosha, kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwemo upimàji na
tiba, kuhakikisha nchi zinatoa mafunzo ya Kutosha kwa watumishi wa afya katika
fani hii.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu akifuatilia mkutano huo. |
Picha ya pamoja ya wake wa marais na mawaziri wa afya wa afrika,waliohudhuria mkutano wa 10 wa kupambana na saratani ya shingo ya Kizazi,matiti na tezi dume (picha/habari na wizara ya afya). |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni