Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari vyombo mbali mbali. |
Katika hali isiyo ya
kawaida shirika la maji safi na maji taka DAWASCO jijini Dar Es Saaal na Pwani
DAWASCO, limeingia mitini
katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina ya
kutembelea
miondombinu ya maji taka na
maji safi Jijini dar Es Salaam na Pwani jana.
Licha ya Shirika Hilo kupewa Taarifa ya Ziara ya Naibu waziri
Mpina mwezi mmoja kabla limekaidi kwa kutoitikia wito huo hata kwa
kumuwasilisha mtumishi mmoja kuwakilisha shirika hilo.
.
Akiongea kwa ukali baada ya kutembelea Bomba la kusafirisha
maji taka kwenda baharini la Ocean road, Naibu Waziri Mpina amesema ubovu wa
bomba la ocean road unatokana na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu, unaonyesha
dhahiri kuwa DAWASCO wana Jeuri kwa IKulu, kwa kutokulifanyia ukarabati kwa
muda mrefu Bomba hilo lililoko karibu na maeneo hayo.
Alipotembelea mabwawa ya maji taka ya mabibo na buguruni, Mhe
Mpina Alisema pamoja na kuwa miondombinu hiyo inaelemewa na wingi wa wakazi wa Dar Es Salaam, Mamlaka husika zina
wajibu wa kuyafanyia usafi mabwawa hayo lakini, hazijaonekana jitihada zozote
za kufanya hivyo, na miondombinu hiyo inaonekana kutofanyiwa ukarabati kwa muda
wa miezi sita.
Naibu Waziri Mpina alisisitiza kuwa ubovu na uchafu wa
miundombinu hiyo unapelekea uchafuzi wa mazingira na hivyo kuhatarisha maisha
ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na viumbe hai wengine.
Akiongea kwa Uchungu, Mkazi mmoja wa Mabibo aliyekataa kutaja
jina lake alisema kuwa, ninanukuu“Mabwawa
haya ni ya Dawasco na hata tukitaka kuunganisha maji taka kwenye mabomba yao
kuelekea kwenye mabwawa wana taka tuwalipe na tunafanya hivyo, wenye viwanda
halikadhalika wanawalipa dawasco kwa kupitisha maji taka yao katika miundombinu
ya dawasco, lakini najiuliza, kwa nini wanakuwa wagumu kuyafanyia ukarabati au
hata kusafisha tuu?. Mwisho wa kunukuu.
Ziara ya Naibu waziri Mpina ya kukagua miundombinu ya
DAWASCO jana Jijini Dar Es Saalam ilihushisha maafisa kutoka DAWASA na Baraza la
taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC na kuwaagiza NEMC, wapitie miradi yote
inayosimamiwa na DAWASCO na kuona kama wanatenda haki katika kutoa huduma kwa
wananchi.
Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina. |
Mwananchi akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni