Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Nida Textile Industries kilichopo Tabata Jijini Dar es Salaam kimetozwa
faini ya shilingi milioni Thelathini kwa kosa la uchafuzi wa
mazingira kwa
kutiririsha maji taka na yenye sumu katika mto kibangu na kuhatarisha maisha ya
mazingira na viumbe hai pamoja na kiwanda
hicho kuwa na mazingira machafu na hivyo kuhatarisha maisha ya wafanyakazi
kiwandani hapo.
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku saba kwa Baraza
la Taifa na Hifadhi na Usimamizi waMazingira NEMC imetokana na ziara ya Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ya
kukagua viwanda na mazingira nchini ambapo sambamba na adhabu hiyo kiwanda
hicho kimetakiwa kufanya usafi mara moja katika mazingira kiwandani hapo,
pamoja kupeleka repoti ya upimaji wa moshi, vumbi litokanalo na makaa ya mawe
na maji yanayotoka kiwandani hapo ili serikali kujiridhisha kama si hatarishi
kwa mazingira.
‘’Ili kujiridhisha NEMC waje nao wachukue vipimo vya maji
haya yanayotiririka ili tuone kama ni salama kwa mazingira na viumbe hai, na
kiwanda kiwasilishe cheti cha utirishaji maji kwa Baraza.” Alisisitiza Naibu
Waziri Mpina.
Kwa upande wake Meneja wa kiwanda hicho Bwana Mohamed Rajabu
alipoulizwa kama ameikubali adhabu hiyo, alitupia lawama kwa NEMC na kusema
kuwa wao ndo walitoa kibali cha athari ya tathimini ya mazingira kwa kiwanda
hicho na ndiyo maana kinaendelea kufanya kazi na kuwa wangekuwa wanapita kwanza
na kutoa onyo kwa wenye viwanda kabla ya kutoa adhabu kali ya mamilioni ya
fedha, na kuongeza kuwa kukabiliana na faini kubwa hivyo kwa kiwanda hicho
kunaweza kupelekea wafanyaki kupoteza ajira zao kwa kupunguzwa kazini.
Akihitimisha
katika zoezi hilo Naibu waziri Mpina aliwataka wawekezaji na wenye viwanda
nchini kutii sheria na kuthamini maisha ya wafanyakazi kwa kuyaweka mazingira
safi na salama.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati)akitembezwa ndani ya kiwanda cha Urafiki Textile mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni