Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
mh. Amosi Makalla amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Waziri mkuu
Mh. Kassim Majaliwa.
Mh. Amosi Makalla
ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Amesema
waziri mkuu ambae anakuja kwa ajili ya kufunga maonesho ya nane nane
anatarajiwa kuwasili jijini Mbeya kesho tarehe 7/8/2016 majira ya saa kumi
akitokea jijini Dar Es Salaam na kuondoka tarehe 9/8/2016 baada ya kukamilisha
zoezi la kufunga maonesho.
Makalla amesema
shughuli atakazozifanya Mh. Waziri baada ya kuwasili Mkoani Mbeya hapo kesho ni
kutembelea Ikulu ambapo atasomewa taarifa na kesho kutwa tarehe 8/8/2016 saa
tatu asubuhi ataelekea katika viwanja vya John Mwakangale ambapo kabla ya
kufunga maonesho hayo atakagua mabanda matano (5) miongoni mwa mabanda hayo ni banda
la Magereza, banda la Pembejeo, banda la Halmashauri na mengineyo.
Hata hivyo amesisitiza
kuwa maandalizi ya kumlaki kiongozi huyo ambae kwa mara ya kwanza anawasili
mkoani hapa tangu aingie madarakani yamekamilika na kwamba viongozi mbali mbali
wakiwemo wakuu wa mikoa tayari wamesha wasili kwa ajili ya zoezi la kufunga
maonesho hayo.
Aidha alimaliza kwa kuwataka
wananchi wa mkoani Mbeya wajitokeze kwa wingi hapo kesho kumlaki mh. Waziri
Mkuu pindi atakapo wasili katika uwanja wa ndege (airpot) sanjari na kujitokeza
kwa wingi katika viwanja vya John Mwakangale ambapo zoezi la kuhitimisha
maonesho ya nane nane yatafanyia.
Maonesho ya nane nane
(8,8) yalianza rasmi tarehe 1/8/2016 ambapo yalizinduliwa na waziri wa Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles John Tizeba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni