Jumatano, 4 Oktoba 2017

UWT KYELA YAADHIMISHA MIAKA 39 , KWA KUTOA MSAADA KWA WAFUNZI YATIMA 35 !!

Mmoja kati ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ngonga iliyopo kata ya Ngonga katika halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya akikabidhiwa sare za shule pamoja vifaa vingine vya masomo!!


Katika kuadhimisha miaka 39 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) iliyo chini ya Chama cha Mapinduzi CCM, Umoja wa Wanawake wa CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiongozwa na mwenyekiti wao Bi. Rhoda Mwamunyange,
wametoa msaada wa vifaa vya shule  kwa watoto yatima 35, wanaosoma katika shule za msingi Ngonga, Mpanda na Maendeleo zilizopo katika kata za Ngonga, Ipyana na Bondeni katika halmashauri ya Wilaya ya Kyela.


Vifaa vilivyo tolewa ni kama Sare za shule, Madaftari, Kalamu, Sabuni na Mafuta vyenye tahamni ya shilingi laki nne na hamsini na saba (457,000), Bi. Mwamunyange amesema wameamua kutoa msaasa kwa watoto hao baada ya kubaini kuwa pamoja na jitihada za serikali kutoa elimu bure lakini bado walezi walio achiwa jukumu la kuwalea watoto hao wanakabiliwa na changamoto ya kushindwa kuwatimizia mahitaji yote kutokana kuelemewa kiuwezo jambo ambalo linawaongezea watoto hao hali ya unyonge, kukata tamaa na hivyo kushindwa kufanya vizuri katika masomo.


Mwamunyange ameongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu na kwamba baada ya kumaliza kutoa msaada katika shule za msingi na sekondari wilayani humo Umoja huo utaendelea kuwasaidia wazee wasio jiweza, kufanya usafi katika maeneo mbali mbali, kutembelea wagonjwa mahospitalini pamoja na kutoa elimu ya athari za mimba za utotoni kwa jamii na wanafunzi.

Hata hivyo amewataka watoto hao kuepuka kujihusiha na makundi yasiyo faa na badala yake wawekeze jitihada zao katika elimu kwa kuwa ndiyo mkombozi wa maisha yao ya baadaye.


Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mpanda Hilda Kajubili, Atupakisye Sungule mkazi wa Kyela pamoja na  Yohana Mwakafwila mwanafunzi wa darasa la sita kutoka shule ya msingi Ngonga ambaye amenufaika na msaada huo wametoa shukrani kwa Umoja wa Wakina mama Ccm kwa kujitolea kuwasaida watoto hao na kuahidi kurejesha fadhila hizo kwa Umoja wa Wakina Mama CCM.
                                                                Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni